UJERUMANI VS ARGENTINA: MTOTO HATUMWI SOKONI LEO,
ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaaa, !!!!!!!!!!!!!!!!!!
NI Ujerumani vs Argentina usiku wa leo.
MIAMBA miwili ya soka duniani, Ujerumani na Argentina inakutana kwa mara nyingine katika fainali za Kombe la Dunia 2014 usiku huu katika Uwanja wa Maracana, Rio de Jeneiro nchini Brazil.Nyota wa Ujerumani aliyeweka rekodi ya upachikaji mabao katika Kombe la Dunia akiwa jumla ya mabao 16, Miroslav Josef Klose.
Ujerumani wametwaa kombe hilo mara tatu mwaka 1954, 1974 na 1990 huku Argentina wakilitwaa mara mbili mwaka 1978 na 1986.Iwapo Ujerumani watashinda watakuwa wamelitwaa kombe hilo mara nne sawa na Italia na iwapo watashinda Argentina watakuwa wamelitwaa mara tatu sawa na Ujerumani.
Orodha ya washindi wa kombe hilo tangu mwaka 1930 ni kama ifuatavyo:
MWAKA
|
MSHINDI
|
1930 | Uruguay |
1934 | Italia |
1938 | Italia |
1950 | Uruguay |
1954 | Ujerumani Magharibi |
1958 | Brazil |
1962 | Brazil |
1966 | England |
1970 | Brazil |
1974 | Ujerumani Magharibi |
1978 | Argentina |
1982 | Italia |
1986 | Argentina |
1990 | Ujerumani Magharibi |
1994 | Brazil |
1998 | Ufaransa |
2002 | Brazil |
2006 | Italia |
2010 | Hispania |
2014 | ? |
ZAWADI
Bingwa wa mwaka huu ataondoka na kitita cha dola milioni 35 sawa na shilingi bilioni 58.2, mshindi wa pili akilamba dola milioni 25 sawa na shilingi bilioni 41.6 huku mshindi wa tatu akikomba dola milioni 22 sawa na shilingi bilioni 36.6 na mshindi wa nne akiweka kibindoni dala milioni 20 sawa na shilingi bilioni 33.3.
Timu nne zitakazoaga mashindano hayo katika hatua ya robo fainali zitachukua dalo milioni 14 kila mmoja sawa na shilingi bilioni 23.3.
Timu nane zilizoondolewa katika hatua ya 16 Bora zitachukua dola milioni 9 kila mmoja sawa na shilingi bilioni 15 na timu 16 zilizoondolewa katika makundi kila mmoja atachukua dola milioni 8 sawa na shilingi bilioni 13.3.
No comments:
Post a Comment