Wanafunzi wa Kampala International University Campus ya Dar es salaam wafanya mgomo
mobomu yatawala
Na Henry Buretta
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa Cha Kampala (KIU) leo
wameandamana na katika chuo hicho kushinikiza warudishe fedha zao kutokana na
kuanzisha kitivo ambacho
hakitambuliki na mamlaka za nchi.
Mgomo huo umeanza majira ya saa tatu kwa baadhi wanafunzi
kuwazuia wenzao wasiingie katika chumba cha mtihani na baada ya hapo wakaibuka
na mabango kwenda katika ofisi za utawala wa chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika chuo hicho,Rais
wa Serikali wa Chuo Kikuu cha Kampala(Kiupeso),Elias Mbogho amesema kuwa
maandamano hayo yametokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu ngazi ya cheti ya
ufamasia kudai leseni na kuambiwa chuo hakitambuliki ndipo chanzo kiliazia
hapo.
Mbogho amesema kuwa hatua mbalimbali zilishapita na
kujiridhisha kuwa kinatambulika lakini wanafunzi wakitivo hicho wameendelea
kuweka malumbano.
Afisa uhusiano wa chuo hicho ,Keneth Uki amesema kuwa mgogoro
huo ulishapewa suluhu kwa kupitia hatua za mamlaka za serikali na kudhibitisha
kutambuliwa chuo hicho.
No comments:
Post a Comment