ZITTO: HAPA NDO NILIPO
Mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa
rasmi uanachama kwa mbunge wa
Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali
pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote
anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa
katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza
rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA.
No comments:
Post a Comment