Wanachuo Dodoma walivyoipindua serikali yao
Mapinduzi
hayo yalifanyika Mei 30 asubuhi ambapo wanafunzi hao walimpindua aliyekuwa
Rais wa kitivo hicho, John Nzilanyingi na kumuweka aliyekuwa waziri wa
afya na mikopo, Simon Mpandalume kuwa Rais wa mpito wa serikali hiyo
hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika Juni mosi mwaka huu.
Rais aliyepinduliwa anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa
kuwakandamiza wanafunzi wenzake kwa kushirikiana na uongozi wa chuo.
Aidha anatuhumiwa kwa ufujaji wa fedha za wanafunzi ambapo anadaiwa
kutumia sh milion 7 za michango ya wanafunzi kununulia gari yake ya
kutembelea.
Mpaka sasa Rais huyo hajulikani alipo kwani baada ya kupinduliwa alitoweka eneo la chuo.
No comments:
Post a Comment